Lulu aweka wazi kuhusu mipango ya harusi yake na Majizo

0
206

Muigizaji wa Bongo Muvi, Elizabeth Michael ‘Lulu’, amefunguka kuwa suala la ndoa yake na mchumba wake, Majizo lipo palepale, kinachosubiriwa ni Mungu aibariki siku hiyo.

Lulu ambaye miaka miwili iliyopita alivishwa pete ya uchumba na mchumba wake huyo, amekuwa akizua maswali mengi kutoka kwa mashabiki wake ambao wengi wamekuwa wakitaka kujua lini atafunga ndoa kwa kuwa ni muda umepita toka alipovishwa pete ya uchumba.

Lulu amesema watu waache kujipa presha kuhoji lini atafunga ndoa, kwa kuwa suala hilo hupangwa na Mungu, huku akiongeza kuwa kila mtu ana mipango katika maisha yake kwa hiyo wao wapo na mipango yao pia kwa kuwa kwa sasa wana vitu vya muhimu wanavyofanya ambavyo vitakuja kudumisha ndoa yao.

“Kukaa miaka miwili ukiwa na pete ya uchumba siyo ishu sana, kwa sababu kila mtu ana mipango yake kwenye maisha, kuna ambao walichumbiana na kuja kuvishana pete baada ya miaka 10’.

Pia Lulu ameendelea kusema kuwa mashabiki wangu na watu wengine wasiwe na wasiwasi, kuna mipango mingine ambayo tunaifanya kwa sasa ambavyo itakuja kudumisha ndoa yetu,” alisema Lulu.

Muigizaji huyo kwasasa yupo kwenye mahusiano ya kimapenzi na mmiliki wa TV E na EFM Fransic Siza maarufu kama DJ Majizo.

LEAVE A REPLY