Lulu atoa msaada wa Pads akiwa gerezani

0
162

Muigizaji wa Bongo Movie, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu ambaye kwa sasa anaendelea kutumikia kifungo chake jela ametoa mchango wake wa Pads kwa lengo la kuwasaidia watoto wa kike.

Zawadi hizo ambazo ziliwakilishwa na msanii mwenzake Dkt Cheni jana baada ya kukabidhiwa na kutoa mchango huo.

Dkt Cheni amesema kuwa anaamini kampeni hiyi itawaweza kuleta mabadiliko makubwa kwenye jamii ya sasa kutoka na matatizo wanayokumbana na watoto wa kike walioko mashuleni.

“Huu ni mzigo wa Elizabeth Michael (LULU), ameomba niwasilishe kwenu. Nimekuwa nikimtembelea mara kadhaa kumjulia hali na yeye ameomba ashiriki kwenye kampeni hii ingawaje hayupo.

Pia Dk Cheni amesema kuwa Lulu amesema awaambie anawapenda sana, na anawataka mabinti wa kitanzania wawe huru katika kutimiza malengo yao, wasikate tamaa na Mungu atawasimamia.

Elizabeth Michael anatumikia kifungo cha miaka miwili jela baada ya kukutwa na hatia ya kumuua aliyekuwa mpenzi wake na muigizaji mwenzake Steven Kanumba bila kukusudia mnamo April 7, 2014.

LEAVE A REPLY