Lulu akanusha kuwa mjamzito

0
99

Muigizaji wa Bongo movie, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu ameweka wazi kuwa sio mjamzito kama watu waavyodai na hata alipotoka gerezani hakuwa mjamzito.

Lulu amefunguka hayo baada ya kuenea tetesi kuwa muigizaji huyo anaujauzito kutokana na muonekano wake wa sasa.

Lulu alitoka gerezani mwaka jana Baada ya kutumikia kifungo kwa miezi kadhaa lakini Baada ya kutoka kuna tetesi zilisambaa kuwa ametoka mapema kutokana na ujauzito na pia alikuwa ameongezeka kwa kiasi kikubwa.

Lulu ameweka wazi kuwa hajawahi kuwa mjamzito kabisa bali alinenepa alipokuwa jela na kuongezeka karibia kilo 20 ambapo kwasasa zimeanza kupungua.

Lulu amesema taarifa zilizowahi kusambaa kuwa alikuwa mjamzito hazily was za kweli bali alivyotoka jela alikuwa ameongezeka kilo 20 hivyo kupelekea mwili Wake kuwa mkubwa sana.

Lakini pia amefungukia tetesi za kugombana na Mpenzi wake Majizzo ambapo amesema kuwa hawezi kuongea chochote kuhusu maisha yake binafsi.

 

LEAVE A REPLY