Lulu aanza kufanya usafi katika jengo la wizara ya Ndani

0
138

Muigizaji wa Bongo Movie, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameanza kufanya kazi ya usafi katika jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani jijijni Dar es Salaam baada ya kutoka jela.

 

Lulu amekuwa akifika makao makuu ya wizara hiyo asubuhi na kufanya majukumu yake na kuondoka mnamo saa 4 au 5 kabla ya mchana.

 

Baada ya kumaliza kazi zake hizo za kufagia na kudeki, Lulu ambaye hufika hapo kwa gari, pia huondoka kwa gari kurejea nyumbani.

 

Mwigizaji huyo alihukumiwa kwenda jela miaka miwili kwa kumuua bila kukusudia mwigizaji mwenzake, Steven Kanumba, lakini adhabu hiyo imebadilishwa na kuwa kifungo cha nje.

LEAVE A REPLY