Lukaku kumfikisha mahakamani mmiliki wa Everton kisa ushirikina

0
82

Mshambuliaji wa Manchester United, Romelu Lukaku atamfikisha mahakamani mmiliki wa Everton Farhad Moshiri kufuatia madai yake kuwa mchezaji huyo aliamua kuondoka baada ya kupata ushauri kutoka kwa mganga wa kienyeji.

Moshiri aliyasema hayo wakati wa kikao cha mwaka cha wamiliki wa hisa za klabu hiyo siku ya Jumanne nakudai kuwa ujumbe huo ulimtaka Lukaku kukataa kupokea ofa mpya ya kiasi cha paundi 140,000 kwa wiki ndani ya Everton na badala yake ajiunge na Chelsea ndipo ghafla akaiambia klabu kuwa anahitaji kuondoka.

Hatimaye akajiunga na Manchester United kwa dili nono la paundi milioni 75, hivyo ndivyo Mushiri ameuambia mkutano huo wa mwaka wa AGM sababu za Lukaku kuondoka.

Lukaku anahisi kuumizwa na Moshiri, kufuatia matamshi yake aliyosema hadharani.  “Tulimpatia ofa nzuri zaidi ya ile ya Chelsea na wakala wake alikuja kwaajili ya kusaini makubaliano hayo,” amesema Moshiri .

Mshauri wa Lukaku amesema kuwa maneno yaliyozungumzwa na Moshiri yamemuaribia taswira ya mchezaji huyo, kwakuwa maamuzi ya Lukaku kuondoka Everton hayahusiani na maswala ya imani za kishirikina  bali yalikuwa ni maamuzi binafsi.

Mshauri amesema kuwa “Sasa ataona hatua zitakazochukuliwa na mahakama na namna mahusiano yao yatavyokuwa, Romelu ni mkatoliki safi na uchawi siyosehemu ya maisha yake na wala hanaimani na maswala hayo,”.

LEAVE A REPLY