Lukaku aweka rekodi mpya Manchester United

0
109

Mshambuliaji wa Manchester United, Romelu Lukaku ambaye amejiunga kwenye klabu hiyo msimu huu lakini ameshatengeneza rekodi ambayo haikuwahi kufikiwa hapo kabla ndani ya timu hiyo.

Mshambuliaji huyo wa Kibelgiji, alifunga mara mbili Jumatano usiku katika mchezo wa Champions League dhidi ya CSKA Moscow na kuendeleza makali yake ya ufungaji.

Lukaku ambaye amejiunga na klabu hiyo akitokea Everton kwa paundi milioni 75 hadi sasa amefunga magoli 10 katika mechi zake 9 za mwanzo za kimashindano.

Hapo kabla, hakuna mchezaji yeyote wa Manchester United aliyefunga idadi kama hiyo katika mechi 9 za mwanzo ndani ya msimu wa kwanza kwa United, hii imefanywa kwa mara ya kwanza na Lukaku.

Kwa kufanya hivyo, Lukaku anavuka rekodi ya Bobby Charlton ya mwaka 1956 ya magoli tisa katika mechi tisa.

 

LEAVE A REPLY