Lowassa na Mbowe wamlilia rais Magufuli

0
1863

Waziri mkuu wa zamani na aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA, Edward Lowassa amewaomba viongozi wa CHADEMA kutobishana na rais Magufuli kwa sasa na badala yake wamjibu wakati wa uchaguzi mkuu mwaka 2020.

Lowassa aliyekuwa kwenye mkutano na wananchi wa Muleba alidai kuwa misimamo ya rais Magufuli haipaswi kujibiwa kwa mabishano ya maneno matupu lakini yajibiwe kwa vitendo ifikapo 2020.

Lowassa alikuwa mkoani Kagera kwaajili ya kuwapa pole waathirika wa tetemeko la ardhi lilitokea mwezi Septemba mwaka jana.

Pamoja na Lowassa kuwaomba viongozi hao kufanya hivyo lakini hakuwa tayari kuiweka wazi misimamo ya rais Magufuli ambayo haipaswi kujibiwa kwa maneno na badala yake wasubiri uchaguzi huo.

Wakati huo huo Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe amemtaka rais Magufuli asaidie kutatua tatizo la uhaba wa chakula kwenye baadhi ya maeneo yanayokabiliwa na njaa nchini.

LEAVE A REPLY