Liverpool ‘uso kwa uso’ na Manchester City robo fainali klabu bingwa Ulaya

0
307

Klabu ya Liverpool itakutana na Manchester City kwenye robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani, Ulaya.

Timu hizo tayari zimekutana mara mbili kwenye ligi kuu nchini Uingereza ambapo kila moja imeshinda mechi ya nyumbani.

Liverpool itaikaribisha Manchester City kwenye mechi ya kwanza itakayofanyika Aprili 3/4 huku mechi ya marudiano ikifanyika Aprili 10/11 mwaka huu katika uwanja wa Etihad.

Manchester City imefuzu nafasi hiyo baada ya kuwafunga FC Basel jumla ya magoli 5-2, huku Liverpool ikitoa FC Porto kwa jumla ya magoli 5-0.

Kwa upande wa bingwa mtetezi, Real Madrid watacheza na Juventus ambapo mechi hiyo itakumbusha fainali ya msimu uliopita.

Sevilla ambayo imeitoa Manchester United itakutana na mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich huku Barcelona itaikabili na AS Roma.

LEAVE A REPLY