Liverpool mpya: Reds 4 Barca 0

0
102

Miamba ya jiji la Liverpool nchini Uingereza, Liverpool wameigalagaza Barcelona ya Hispania kwa mabao 4-0 kwenye uwanja wa Wembley.

Mchezaji aliyeigharimu Liverpool, £34m Sadio Mane alitumia mechi hiyo kufungua kitabu chake cha mabao kwenye klabu yake mpya kwa kuifungia la kwanaza kwenya dakika ya 15 kabla ya kiungo wa zamani wa Liverpool na timu ya taifa ya Argentina, Javier Mascherano kujifunga.

Mechi hiyo ya mashindano ya kimataifa ya International Champions Cup ni maalum kwaajili ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi.

Wachezaji Divock Origi and Marko Grujic pia waliifungia bao moja kila mmoja na kuufanya ushindi wa jumla wa timu yao kuwa 4-0.

Barcelona iliyokuwa na mastaa wao wa dunia, Lionel Messi na Luis Suarez haikuonekana kuwa tishio kwa mabeki wa Liverpool kwenye mechi ambayo watazamaji waliweka rekodi ya kufikia 89,945 na hivyo kuwa idadi ya pili kwa ukubwa kufikiwa kwenye uwanja huo.

Kwenye mechi hiyo kiungo wa Liverpool James Milner alitolewa kabla ya mapumziko baada ya kuumia mguu.

LEAVE A REPLY