Liverpool kuikaribisha Manchester United leo

0
81

Licha ya kuwa Kocha Jose Mourinho amekuwa na rekodi nzuri ya kuifunga Liverpool, lakini nguli wa Liverpool, Kenny Dalglish anaamini kocha huyo ataingia uwanjani leo kwenye Uwanja wa Anfield na ‘kupaki basi’.

Mourinho akiwa anaiongoza Manchester United, watakipiga na wapinzani wao hao katika Premier League na tayari presha imekuwa kubwa kuelekea mchezo huo.

United imekuwa na kasi kubwa ya kufunga mabao ambapo imeshapata ushindi wa mabao manne katika mechi sita za hivi karibuni lakini hilo siyo kitu kwa nguli huyo kuamini kuwa United itaingia kushambulia.

Dalglish amenukuliwa akisema: “Miaka mitatu iliyopita Jose akiwa na Chelsea aliifanya kazi hiyo ya kuzuia vizuri walipokuja hapa (Anfield), naamini hata sasa atafanya hivyo pia.

LEAVE A REPLY