Linex afunguka kuachwa na mpenzi wake

0
120

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Linex Sunday Mjeda amemshukuru mpenzi wake wa zamani aliyeamua kumuacha, hadi ikapelekea kuandika wimbo wa Mama Halima, ambao ulifanya vizuri kipindi cha nyuma.

Linex amesema asingeachwa na mwanamke huyo asingejua hatma yake leo hii angekuwa wapi mana amejiufunza vitu vingi.

“Popote ulipo Halima nakushukuru sana kwa sababu kunitupa kwako kulisababisha niandike wimbo mzuri ambao utafanya uishi milele, hata kesho nikiwa sipo watu watasikiliza, nakubaliana na kuniacha kwako, sio lazima kila mtu awe adui yako na asingeniacha sijui leo hii ningekuwa wapi mimi, ahsante mama” ameeleza Linex.

Linex amewataka wanawake kuacha tabia ya kuwaita wanaume wasiowajua jina la kaka, kama sio ndugu zao kwa sababu muda mwingine huwa wanajizibia riziki za kupata wachumba.

Pia ameengenza kwa kusema kuwa “Wanawake waache kutuita wanaume Kaka zao kama sio ndugu zao, muda mwingine mnazuia ridhiki  bure tu,  kwa mfano mimi natokea Kigoma utakuta mwanamke wa Moshi ananiita Kaka, je kama nataka nijiongeze kwake itakuaje”.

LEAVE A REPLY