Linah Sana afungua studio ya muziki

0
323

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Linah amefunguka na kusema kuwa amefungua studio yake ya kurekodia muziki lakini hafikrii siku za mbele kuja kuwa producer wa studio hiyo.

Linah amesema kuwa msanii kufanya kazi ya kuimba na kuwa producer inakuwa ngumu ndio maana kuna watu wako maalumu kama mproducer na wengine wako maalumu kama wasanii.

Linah ameendelea kusema kuwa studio hiyo itasaidia wasanii wengine kwa ajili ya kurekodi nyimbo katika studio yake.

Pia amesema kuwa kitu kinachosababisha ukimya wake ni malezi baada ya kujifungua mtoto wake wa kwanza wa kike miezi michache iliyopita.

Lina anaungana na wasanii wa Bongo Fleva ambao wanamiliki studio kama vile Nahreel, Quick Rocka, Rayvanny pamoja na Baucha.

LEAVE A REPLY