Linah apitia changamoto za malezi

0
268

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Linah amefunguka na kusema kuwa inamuumiza sana kumlea mtoto wake akiwa mwenyewe bila malezi kutoka kwa baba yake.

Kauli ya mwanamuziki huyo imekuja baada ya kukosa malezi ya mwanawe kutoka kwa baba yake baada ya kuachana toka mwaka wa jana.

Linah amesema kuwa kama mzazi, inamuumiza sana kulea akiwa peke yake, kwa sababu muda mwingine mtoto anahitaji kuwa karibu na baba yake, hiyo inamuathiri sana mtoto katika ukuaji wake.

Amesema kuwa “Kulea mtoto nikiwa peke yangu inaniumiza sana, maana mtoto anaweza akaamka akamuhitaji baba yake, na muda huo baba hayupo, hiyo inaniumiza sana kwa mtoto wangu, na inaniathiri hata katika muziki wangu maana naelemewa na majukumu,”.

Mwanamuziko huyo kwasasa ameanzisha mahusiano na mwanaume mwingine aitwae DJ Seven ambaye ni official DJ wa Mwanamuziki Harmonize.

LEAVE A REPLY