Linah akataa ndoa

0
117

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Linah Sanga amefunguka na kuweka wazi kuwa hivi sasa hana mpango wa kuolewa na wala hawazi kuhusu mambo ya ndoa.

Linah amefunguka kuwa maisha ya ndoa kwa sasa hayafikirii na badala yake anatamani kuona muziki wake unampa heshima kwanza.

Linah amesema, licha ya wanawake wengi kutamani ndoa lakini kwake inekuwa tofauti na badala yake ameelekeza nguvu zaidi kwenye kazi zake.

Linah amezaa mtoto mmoja na mwanaume ambaye alikuwa kwenye mahusiano naye ya muda mrefu aitwaye Shaban Mchomvu ambaye amezaa naye Mtoto mmoja wa kike anayeitwa Tracey Paris.

LEAVE A REPLY