Linah ajivunia kuwa mama

0
365

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Linah Sanga amefunguka na kusema anajivunia sana kuwa mama na anamshukuru Mungu kwa kumpa zawadi hiyo ya mtoto.

Linah amesema kuwa baada ya kupata mtoto huyo amebadilika sana na kuwa mama hivyo ameongeza kitu katika maisha yake.

Lina alifanikiwa  kujifungua mtoto wake wa kwanza ambaye anaitwa Tracey Paris mapema  mwaka jana na mpenzi wake wa siku nyingi Director Ghost.

Linah amesema kuwa hapendelei kukaa mbali na mwanaye huyo wa kike aitwaye Trecy kwa muda mrefu kwa kuwa mtoto anapaswa kuwa jirani na mama ili aweze kuwa na mapenzi na mama yake.

Kwasasa msanii huyo yupo kwenye muziki ikiwa single yake ya mwisho kutoka ilikuwa ni ‘Same Boy’ aliyoshirikiana na Rachelo.

LEAVE A REPLY