Linah ajifungua mtoto wa kike leo

0
415

Mwanamuziki wa Bongo fleva, Lina Sanga leo amejifungua mtoto wa kike katika hospitali ya Maria Stopes iliyopo Mwenge jijini Dar es salaam.

Kabla ya kupata ujauzito kutoka kwa baba mtoto wake anayejulikana kama director Ghost, huko nyuma Linah aliwahi kupata misukosuko baada ya mimba aliyopewa na mpenzi wake wa zamani kutoka.

Ila leo hii Linah amewafanyia furaha wengi kuleta kiumbe duniani ambapo anaendelea vizuri pamoja na mtoto wake.

Wasanii mbalimbali kupitia mitandao ya  kijamii wametumia akaunti zao kumpongeza Linah kwa kujifungua salama mtoto wa kike.

LEAVE A REPLY