Linah afunguka mazito kuhusu wasanii wa kike nchini

0
654

Msanii wa Bongo Flava Linah Sanga, amesema wanamuziki wa kike wana wivu sana ndio maana hawapeani ushirikiano wa kutosha katika kazi kitu kinachopelekea wao kutoendelea.

Linah ameeleza kuwa wanamuziki wa kike wanashindwa kusaidiana kwasababu wanaogopa kuzidiana, na pia wanaona kwamba mmoja akimsaidia mwingine ataonekana anamkubali sana hivyo inapelekea kila moja kutaka kufanya kazi kivyake.

 

Linah ameendelea kusema tatizo hili ndio linapelekea kuwa na wasanii wakike wachache sana katika soko la muziki, kwasababu hata wale waliotangulia kuingia kwenye tasnia hiyo wanakuwa wagumu kusaidia wengine wakihisi kwamba ndio itakuwa chanzo cha kushuka kwao kimuziki.

 

Linah amewashauri wanawake wenzie kuungana na kuwa kitu kimoja ili waweze kupeleka muziki wao mbali,aliongeza kuwa upendo ni bora sana katika kazi na wasiishi kwa kuogopana.

LEAVE A REPLY