Linah afunguka mahusiano yake na Amini

0
184

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Linnah amefunguka na kusema kuwa aliumia sana alivyoachana na msanii Amini kwasababu alikuwa anampenda.

Linnah amesema kuwa aliumia sana alivyoachana na mpenzi wake huyo wa zamani Amini mpaka kuamua kuanzisha mahusiano na mwanaume mwengine.

Pia kuhusu uhusiano wa sasa baina ya wasanii hao ambao chimbuko lao ni THT, Linnah amesema kuwa atatafuta wakati rasmi wa kutambulisha penzi lao, lakini kwa sasa watambue tu kuwa wako pamoja na lolote linaweza kutokea.

Amini na Linnah kwa pamoja wametambulisha ngoma ya pamoja inayojulikana kama ‘Nimenasa’.

Taarifa za kurejea kwa penzi la wawili hao lilianza kusambaa hivi karibuni, ikiwa ni baada ya Amini kuachana na mkewe na Linnah kuachana na baba wa mtoto wake hivi karibuni.

LEAVE A REPLY