Linah adai hawezi kubadili dini, wataoana hivyo hivyo na mzazi mwezake kila mtu na dini yake

0
193

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Linah Sanga amesema kuwa ni vigumu sana kwa mtu kubadili dini sababu ya mapenzi kutokana na wazazi wa pande zote mbili.

Kauli hiyo ya Linah imekuja baada ya kukumbana na maswali mengi kuhusu mzazi mwezake ambaye dini zao ni tofauti, Linah akiwa mkristo na mwenzake akiwa muislamu.

Mwanamuziki huyo ambaye ni zao la THT amesema kuwa kubadili dini iwe sababu ya Mwenyenzi Mungu tu lakini siyo masuala ya kimapenzi kutokana mnaweza kuachana kwenye mapenzi yenu.

Lina ameendelea kusema kuwa  hata akibadilisha dini ni kwa sababu ya Mungu siyo kwa sababu ya mapenzi kutokana na hayo akutaka kufanya hivyo.

 Kuhusu kubadili dini Linah amesema kuwa kwao ndio kuna tatizo kubwa sana japo mpenzi wake ni pia ngumu.

Kutokana na hayo Lina amesema kuwa yeye na mzazi mwenzake wataoana hivyo hivyo kila mtu na dini yake na kama upande mmoja utakubali kubadilisha watafanya hivyo kwasababu hawawezi kuachana sababu ya dini.

LEAVE A REPLY