Lil Wayne azindua albam yake mpya

0
370

Mwanamuziki wa Marekani, Lil Wayne amezindua albam yake ya mpya iitwayo The Carter V  ambayo imemchukua miaka ipatayo sita kuiachia kutokana na masuala ya kisheria.

Wayne alisema anasikitika hakuweza kumshirikisha mwanamuziki Drake katika albam hiyo kutokana na masuala ya kisheria, japokuwa alimshirikisha kikamilifu siku ya uzinduzi.

Albam hiyo yenye nyimbo 23 inawajumuisha wanamuziki Kendrick, Travis Scott, Nicki Minaj, Sampha, Snoop Dogg, na wengine wengi.

Albamu ya mwanamuziki huyo ilichelewa kutoka kutokana na kutoelewana na uongozi wa iliyokuwa lebo yake Cash Money.

LEAVE A REPLY