Lil Wayne akatisha show ghafla jukwaani

0
57

Mwanamuziki nyota wa rap nchini Marekani, Lil Wayne amekatisha show yake ghafla mjini Atlanta baada ya kusikika sauti ikisema piga risasi wakati akitumbuiza jukwaanii usiku wa kuamkia leo.

Baada ya sauti hiyo watu waliohudhuria show hiyo walishikwa na taharuki na kuanza kukanyagana wakigombania kutoka nje wakidhani ni sauti ya makundi ya kialifu au kigaidi.

Lakini hadi sasa haijathibitishwa kama sauti ile ilitolewa na nani na walikuwa na nia ya kushambulia jukwaani hapo au mtu aliamua tu kutoa sauti kama hiyo.

Inasemekana watu mia moja wamepata majeraha kwenye tukio kutokana na kukanyagana huku watatu wakianguka kwa mshtuko.

Hii ni show ya kwanza kwa Lil Wayne kufanya tangu aachie Album yake ya ‘Tha Carter V’ wiki iliyopita baada ya vuta nikuvute na kundi lake la Cash Money.

LEAVE A REPLY