Lil Ommy atajwa kuwania tuzo nchini Marekani

0
27

Mtangazaji wa vipindi vya The Switch na Big Sunday vya Wasafi FM, Lil Ommy, ametajwa kwa mwaka wa pili mfululizo kuwania Tuzo za African Entertainment Awards (AEAUSA) zinazotolewa Marekani kama Mtangazaji Bora Afrika.

Oktoba 2019, Lil Ommy aliibuka mshindi kwenye tuzo hizo, hivyo hadi sasa ndiye anayeshikilia nafasi hiyo inayowaniwa tena, kama Mtangazaji Bora Afrika, akiiwakilisha vyema Tanzania.

Lil Ommy amesema kuwa yeye ndiye Mtangazaji pekee wa Tanzania anayewania tuzo hiyo, anawaomba Watanzania wote wampigie kura ili Tanzania ishinde. Pia, amewashukuru tena kwa kumpa ushindi mwaka jana, akieleza kuwa “Tanzania ilishinda”.

Katika hatua nyingine, DJ Sinyorita wa Clouds FM, amechaguliwa kwa mara ya kwanza kuwania Tuzo ya DJ Bora Afrika katika tuzo hizo. Ni DJ wa kike na mtanzania pekee anayewania tuzo kwenye kipengele hiki.

Lil Ommy mtanzania anawania tuzo hizi bila kuwa mwanamuziki, wakiwakilisha kiwanda cha burudani kama mtangazaji wa vipindi.

LEAVE A REPLY