Ligi kuu, EFL na FA zaanzisha sheria mpya kudhibiti tabia za wachezaji

0
145

Chama cha soka cha Uingereza na bodi zinazosimamia mchezo huo nchini humo vimeanzisha sheria mpya ya kadi nyekundu kwa wachezaji na maafisa wa vilabu ikiwemo makocha ili kudhibiti kile walichokiita ‘tabia zisizovumilika’

Taarifa ya pamoja ya kamati ya Ligi Kuu ya Uingereza, kamati ya Ligi daraja la kwanza na chama cha soka inasema kuwa matendo yasiyofaa kwenye soka yamefikia hatua isiyovumilika hivyo kuanzia msimu mpya wa ligi kadi nyekundu itaonyeshwa kwa mchezaji watakaowakabili waamuzi na matumizi ya lugha ya matusi au kuwaonyesha ishara mbaya waamuzi.

Tabia za utovu wa nidhamu kwenye maeneo ya wachezaji wa akiba na walimu pia zitashughulikiwa na sheria hiyo mpya.

Mwenyekiti wa ligi kuu Richard Scudamore amesema kwa muda mrefu sasa kumekuwepo na hali ya wachezaji kuvuka mipaka yao.

Hivyo ni msimamo wetu wa pamoja kuwa tabia hizi hazipaswi kuvumiliwa tena.

Makosa mapya yanayopelekea mchezaji kupata kadi ya njano ni:

  • Kuonyesha wazi tabia ya kutowaheshimu waamuzi wa mechi
  • Kufanya fujo katika kupinga uamuzi wa refarii
  • Kumkimbilia refa kwa fujo kupinga uamuzi wake
  • Kutukana au kutumia lugha ya kuudhi na/au ishara ya kuudhi kwa waamuzi
  • Kadi ya njano kwa angalau mchezaji mmoja pindi wachezaji wanapomzunguka mwamuzi
  • Kugusana na mwamuzi katika hali isiyoashiria fujo

Makosa mapya yanayopelekea mchezaji kupata kadi nyekundu

  • Mchezaji kumkabili mwamuzi na kumfanyia maudhi au kutumia lugha ya matusi au lugha ya kuudhi na/au ishara ya kuudhi kwa mwamuzi
  • Kugusana na waamuzi kwa fujo au kukabiliana nao kwa namna ya fujo

LEAVE A REPLY