Lema awaonya watu wanaotaka kumteka

0
250

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amewaonya watu aliodai kuwa wamemuweka kwenye orodha ya wabunge kumi na moja wanaotakiwa kutekwa.

Lema amedai kuwa yeye haogopi vitisho vya kutekwa na kwamba wanaopanga kumteka wanapaswa kufahamu kuwa hawatafanikiwa na kwamba hakuna atakayeweza kusababisha kifo chake isipokuwa Mungu pekee.

“Ninawaonya watekaji, kwamba ninamjua Mungu ninaemwamini, kwamba hawataliona kaburi langu wala mauti yangu kwa sababu Mungu ninayemuamini najua nguvu zake na najua uwezo wake,” alisema Lema.

“Kwahiyo mimi kutekwa haitawezekana, kuuawa na mtu haitawezekana kwa sababu namtumaini Mungu kwa nguvu zangu zote,”.

Kauli hiyo ya Lema imekuja kufuatia kauli ya Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe aliyeeleza jana Bungeni kuwa alionywa na baadhi wa watu wakiwemo mawaziri kuwa yeye ni miongoni mwa wabunge kumi na moja walio kwenye mpango wa kutekwa na genge la watu wasiojulikana.

LEAVE A REPLY