Leicester City yataka kumuongezea mshahara Mahrez ili abakie klabuni hapo

0
137

Mabingwa wa Ligi Kuu nchini England, Leicester City bado inaendelea kupambana ili kulinda kikosi chake kilichoisaidia kutwaa Ubingwa huo kisibomolewe,  baada ya Leicester City kutwaa taji vilabu vingi vikubwaEngland vinahangahika kuhakikisha vinasajili nyota wa kikosi hiko.

 

Leicester City wameamua kumuongezea mshahara winga wa kimataifa wa Algeria anayeichezea klabu hiyo Riyad Mahrez ili asishawishike kujiunga na Arsenal ambao nao wamepanga kumlipa mshahara wa paundi 100,000 kwa wiki, hivyo Leicester City wanataka kumlipa mshahara huo ili asiondoke.

 

Riyad Mahrez ambaye ni mchezaji bora wa PFA, anawindwa na Arsenal na tayari wameripotiwa kuwa wapo tayari kutoa paundi milioni 37 kwa Leicester City ili wampate nyota huyo, ambaye aliwahi kukaririwa kwa wiki za hivi karibuni akisema kuwa bado hajajua msimamo wake kuhusu kuondoka au kubaikia katika klabu hiyo

LEAVE A REPLY