Lavalava akusha kutoa kimapenzi na Irene Uwoya

0
119

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Lavalava amekanusha tetesi zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kuwa anatoka kimapenzi na muigizaji wa Bongo Movie, Irene Uwoya.

Lava Lava ameamua kusema hayo baada ya taarifa za wawili hao kuwa katika mahusiano zinazidi kusambaa katika mitandao ya kijamii jambo ambalo limeonekana kumkera sana mwanamuziki huyo mpaka kufikia hatua ya kukanusha.

Mwanamuziki huyo lebo ya WCB amesema kuwa tetesi hizo si za kweli wao ni marafiki tu wa kawaida na hakuna kingine kinachoendelea zaidi ya urafiki wao hivyo watu waache kuongea mambo wasiyoyajua.

Lava Lava amesema kuwa kuonekana kwao wakiwa pamoja ndiyo kumeleta maswali yote katika mitandao ya kijamii lakini hakuna kinachoendelea kati yao kwani Irene ni mtu wake wa karibu sana.

Lavalava hajawahi kuanika mahusiano yake na amekuwa akihusishwa kutoka na watu tofauti tofauti lakini amekuwa mtu wa kukanusha tetesi hizo kila apoulizwa kuhusu suala hilo.

LEAVE A REPLY