Lavalava akataa kumuweka hadharani mpenzi wake

0
200

Msanii wa Bongo Fleva anayefanya vizuri chini ya Lebo ya WCB, Abdul maarufu kama Lavalava amefunguka na kuweka wazi kuwa hawezi kumuanika Mpenzi wake hadharani.

Lavalava amejibu kwamba haoni ulazima wa yeye kumuonesha mchumba wake kwasababu sio malengo yake na itaharibu kabisa mfumo wa muziki wake kwasababu watu watavumisha sana.

“Nadhani sio lazima sana watu kujua uhusiano wangu kwasababu hayo ni mambo yangu binafsi jamani yaani kama ningekuwa sijatoa ngoma kwa muda mrefu basi ingekuwa ni haki y a o kuhoji lakini uhusiano wangu hauwahusu kwasababu malengo yangu ni kufanya muziki wangu ujulikane zaidi kuliko mahusiano yangu,” alisema Lavalava.

Tofauti na wasanii wenzake wa WCB, Lavalava pekeee Ndiye ambaye amekuwa akimficha Mpenzi Wake na haijawahi kujulikana ana mahusiano na mwanamke gani tangu alipopata umaarufu.

LEAVE A REPLY