Lava Lava: Mimi si mtu wa totozi kama wengine

0
1133

Mwanamuziki wa Bongo Fleva kutoka ‘WCB’, Lava Lava amefunguka na kusema kuwa yeye si mtu wa kupenda wanawake kama walivyo wanamuziki wenzake.

Lava Lava amesema kuwa kwa upande wake yeye apendelei mambo hayo kwani kila mtu ana tabia yake hivyo ni vigumu kwa yeye kutoka kimapenzi na wanawake tofauti tofauti.

Kuhusu kuwa katika mahusiano, Lava Lava amesema kuwa yupo katika mahusiano ila hapendelei kuweka wazi mahusiano yake kwani anapendelea kufanya vitu kimya kimya bila kuweka public masuala yake ya kimapenzi.

Pia amesema kuwa kuweka mahusiano yake wazi kunaweza kusababisha matatizo katika jamii kutokana na baadhi ya mashabiki zake wengine kutopenda tabia hizo.

Mwanamuziki huyo ni mmoja wa wasanii wanaofanya vizuri katika lebo ya WCB inayoongozwa na mwanamuziki Diamond Platnumz.

LEAVE A REPLY