Lava Lava akanusha kutelekeza mtoto

0
323

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Lava Lava amekanusha tetesi zilizoenea mitandaoni kuwa ametelekeza mtoto ambapo amesema kuwa habari hizo zilisambazwa kumchafua.

Kauli ya mwanamuziki huyo imekuja baada ya kushambuliwa na baadhi ya mashabiki wake kuwa amefanya kitendo kisichokuwa cha kiungwana cha kutelekeza mtoto wake wa kumzaa.

Lava Lava amesema kuwa uvumi huo hata yeye alisikia na kuona baadhi ya video ambazo zilivujishwa kama ushahidi juu ya uhusiano wake na mwanamke aliyedai kuzaa naye.

Lava Lava ni mmoja kati ya wasanii kutoka WCB watakaokinukisha katika shoo ya kwanza ya Wasafi Festival itakayofanyika Mtwara katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona Novemba 24, mwaka huu.

Tamasha hilo litakuwa la kihistoria maana itahusisha wasanii wote kutoka katika Lebo ya Wasafi akiwemo Diamond Platnumz, Harmonize, Mbosso, Queen Darleen pamoja na Rayvanny.

LEAVE A REPLY