Lady Jay Dee: Siwezi kuachia nyimbo kila mara

0
96

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Lady Jay Dee amefunguka na kusema kuwa hawezi kuachia nyimbo mpya kila mara kwasababu nyimbo ni za hisia ambazo zinaweza kudumu miaka mingi.

Jay Dee ameeleza hayo baada ya kuwepo wimbi kubwa la wasanii wakikimbizana kila uchao kutoa tungo mpya kwa mashabiki zao hata kama kazi ya awali haijakaa muda mrefu sokoni.

Jide amesema kuwa “Siwezi kutoa nyimbo mpya kila siku, kwa sababu nyimbo zangu ni za hisia, ambazo zinaweza kuishi hata miaka 10. Ni bora nitoe wimbo mmoja kwa mwaka lakini uwe unaishi miaka mingi kwa ladha ile ile siku zote,”.

Pamoja na hayo, Jay Dee amesema wasanii wengi wa kike wanashindwa kupambana katika muziki kutokana na kutopewa ushirikiano wa kutosha katika kile wanachokifanya japokuwa muda mwingine uongozi nao unachangia.

Mwanamuziki leo ameachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la ‘I miss you’ uliotengenezwa na Man Water.

LEAVE A REPLY