Lady Jay Dee awajia juu waliombeza kuhusu vazi lake

0
150

Mwanamuziki wa Bongo Fleva Judith Wambura maarufu kama a Lady Jay Dee amewajia juu watu ambao wamemsema baada ya picha ya gauni la wazi kusambaa.

Lady Jay Dee alizua gumzo kwenye Mitandao ya kijamii Baada ya picha yake iliyomuonyesha akiwa amevaa gauni jeusi lililoacha sehemu kubwa ya maungo yake nje.

Kupitia akaunti ya Instagram ameandika “Hivi wale watu wa maadili Mbona picha za Hivi huwa hamlike wala hamcomment kwa wingi mkiwekewa?

 Pia ameandika kwa kuandika “Haya maadili hayo hapo sasa inakuwaje? Mbona hamsifii, ila binadamu ni wanafiki sana sijapata kuona”.

Mashabiki walimjia juu Jay D kwa kuvaa nguo iliyomuacha wazi huku wengi wakidai wamechukizwa kwa sababu ni msanii na pia ni Koop cha jamii.

Baada ya Povu hilo Jay Dee ametoa majibu kwa watu hao na kusema wengi wao ni wanafiki kwani hata akivaa mavazi ya heshima huwa hawampongezi pia.

LEAVE A REPLY