Lady Jay Dee afunguka siri ya kufanya vizuri kwenye muziki

0
256

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva,  Lady Jay Dee amefunguka sababu ya kuendelea kufanya vizuri kwenye muziki tofauti na wasanii wengine.

Jide amesema kuwa kitendo cha yeye kuendelea kufanya vizuri kwasababu hakulewa sifa kutokana na umaarufu wake.

Mwanamuziki huyo amesema kitendo hiko kimemfanya aendelee kufanya vizuri na kuendelea kuliteka soko la muziki ndani na nje ya nchi.

Jide amesema kuwa hiyo ndiyo siri pekee iliyomfanya aweze kupita katika vipindi vyote vigumu mpaka leo hii bado yupo katika soko na kuendelea kufanya vizuri licha ya kuanza muziki muda mrefu.

Staa huyo amesisitiza kwa kusema kuwa amekuwepo kwenye muziki takribani miaka 17 bila ya kushuka katika muziki kwa sababu ya kutolewa sifa na kufanya vitu vya tofauti kila siku.

Pia mwanamuziki huyo amesema kuwa Machi 31 anatarajia kuzindua albamu yake mpya ambayo itakuwa ya saba tangu aanze kufanya muziki ndani ya miaka 17.

 

LEAVE A REPLY