Lady Jay Dee afanya shoo ya kibabe mlimani City

0
20

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Lady Jay Dee amefanya shoo akisherehekea kutimiza miaka 20 kwenye muziki wake.

 

Shoo hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na mashabiki kibao waliokuja kumsapoti mwanamuziki huyo.

 

Shoo hiyo ilihudhuriwa na mastaa mbalimbali wa Bongo muvi, Bongo Fleva na wengine ambapo Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) Geofrey Mungereza a.k.a Mzee wa Rungu la Maadili naye alikuwepo akiifutilia kiumakini shoo hiyo.

 

Baadhi ya mastaa walihudhuria ni wasanii wa Bongo Movie, Kajala Masanja, Steve Nyerere, Mwanamitindo Flaviana Matata na wengine wengi.

 

Lady Jay Dee maarufu kama Komando ameanza kuimba muziki wa Bongo Fleva mwaka 2000 na mpaka sasa ametimiza miaka 20 ndani ya game hiyo ya muziki.

LEAVE A REPLY