Lady Jay Dee aachia rasmi albam yake

0
36

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Lady Jay Dee ameachia rasmi albam yake mpya inayokwenda kwa jina la 20 ambayo ina jumla ya nyimbo 20 ambapo uzinduzi wake ulifanyika Februari 12.

Jide ameachia album yake hiyo ilikiwa sehemu ya kuadhimisha miaka 20 ya uwepo wake katika kiwanda cha muziki.

Album hiyo inayopatikana kwenye platforms mbalimbali za kusambaza muziki Duniani, imekamilishwa kwa jumla ya nyimbo 20 zilizobeba uandishi wenye ujumbe na Burudani.

Hata hivyo, Jide anaachia album yake hii ikihesabika kuwa tayari ameutumikia muziki nusu ya umri wa maisha yake mpaka sasa.

Jide ameachia album yake hiyo ikiwa ni kusherehekea miaka yake 20 ya kuwa kwenye kiwanda cha muziki Tanzania “Bongo Flava” huku album hiyo ikiwa imebeba nyimbo 20 na kolabo zikiwa ni 11 tuu.

LEAVE A REPLY