Lady Gaga aanguka jukwaani

0
263

Mwanamuziki wa Marekani, Lady Gaga ameangukia mashabiki wakati wa onyesho la Muziki wake jijini Las Vegas nchini Marekani.

Nyota huyo alimuita shabiki wake kwa jina Jack kujumuika naye jukwaani na kumrukia mikononi mwake- Lakini Jack hakuwa imara na wawili hao walianguka chini.

Badala yake, Lady Gaga alirejea na kutumbuiza kibao chake kiitwacho Million Reasons akiwa sambamba na shabiki huyo anayekwenda kwa jina la Jack.

Mashabiki walikuwa wakifuatilia hali ya Gaga kwa kuwa ana matatizo ya baridi hali inayomsababishia maumivu makali sana.

Mwaka 2013, aliahirisha onyesho lake la Born This Way baada ya kuteguka nyonga. Lakini muimbaji huyo aliwapa moyo mashabiki wakati walinzi walipomsaidia kunyanyuka.

Pia Nyota huyo alimpa moyo Jack, ambaye alikuwa akilia baada ya tukio hilo. ”Usiwe na wasiwasi, kila kitu kiko sawa. si makosa yako,” aliongeza: ”Unaweza kuniahidi kitu? unaweza kuacha kujilaumu kwa kile kilichotokea?”

Baadae kwenye onyesho hilo, Gaga alithibitisha kuwa ajali hiyo haijasababisha madhara yoyote, alipotumbuiza kibao chake, Bad Romance.

LEAVE A REPLY