Kwa kauli hii, King Kiba ‘anataka kufika anapotaka mapema zaidi’

0
609

Staa wa Bongo Fleva, Ali Kiba a.k.a King Kiba ameiweka wazi mipango yake ya kufanikiwa kwenye muziki wake ‘its amazing’.

Kiba ambaye alikuwa akiwania tuzo ya collabo bora zaidi kupitia ngoma ya kundi la Sauti Soul ya ‘Unconditionally Bae’ ambayo yeye ameshirikishwa.

Kiba ameonyesha ukomavu mkubwa kwa kurejea kwenye msemo ‘Ukitaka kufika mbali, nenda na wenzako’ LAKINI ‘Ukitaka kufika haraka nenda peke yako’.

Ali Kiba amedai kuwa ‘Collabo’ haipo kwenye mikakati yake ya kumsaidia kukua kimuziki.

Collabo ni kwaajili ya wasanii wasiojiamini zaidi, ni kwaajili ya wasanii wanaotaka kuingia kwenye soko jipya la muziki kwa kupitia migongo ya watu wengine.

Hiyo haimaanishi kuwa Ali Kiba hayupo tayari kufanya collabo lakini inamaanisha kuwa ‘hajajiandaa kisaikolojia kuandika nyimbo na kuituma menejimenti yake kumtafutia watu au wasanii wakubwa ili afanye collabo. Endapo ataombwa kufanya collabo na wasanii wengine atatazama uwezekano wa kufanya nao.

Kiba kwa kauli hii, ‘umepevuka’ lakini una kitu cha kuthibitisha na si kingine isipokuwa kutoa ngoma kali ‘tupu’ kuthibitisha kuwa ‘Alone yo can stand and alone you can shine’.

Amini Kiba, ukifanikiwa katika hili ‘Legacy yako itaishi milele kwenye Bongo Fleva’.

All the best!!

LEAVE A REPLY