Kusah akanusha kutoka kimapenzi na Aunty Ezekiel

0
31

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Kusah amekanusha kutoka kimapenzi na muigizaji wa Bongo Movie Aunty Ezekiel baada ya wawili hao kuonekana kuwa karibu sana.

Kusah ambaye ni mzazi mwenzie na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ruby amesema kuwa anashangaa watu kusambaza habari hizo wakati hana mahusiano ya kimapenzi na muigizaji huyo licha ya kuwa karibu hivi karibuni.

Kusah amesema wanza kabisa maneno mi nayasikia, lakini mimi Aunty Ezekiel sio mpenzi wangu na hana ujauzito wangu na sijui hata hivyo vitu vinatokea wapi. Labda kwa sababu ananisupport, lakini hakuna kitu chochote kinachoendelea kati yetu,” alisema.

Pia Kusah amesema hajamuelewa Shamsa Ford kwa alichoongea kwa sababu hata kama kweli angekuwa na mahusiano na Aunty kusingekuwa na tatizo lolote kwa sababu Aunty hana ukubwa huo.

LEAVE A REPLY