Kundi la Jabhat al-Nusra lajitenga na Al-Qaeda

0
100

Kiongozi wa kundi la wapiganaji wa Jabhat al-Nusra au kwa jina jengine Nusra Front, Abu Mohammed al-Julani, kupitia ujumbe wa video uliorekodiwa ametangaza kuwa jina la kundi hilo limejiengua kutoka kundi la Al-Qaeda na sasa limebadilishwa jina na litaitwa Jabhat Fateh al-Sham.

Abu Mohammed al-Julani amesema kuwa hatua hiyo imekuja ili kuondoa sababu inayotumiwa na mataifa makubwa ya Magharibi ikiwemo Marekani na Urusi ya kuishambulia kwa mabomu nchi ya Syria.

Wakati huo huo Marekani imejibu kwa kusema kuwa haioni sababu ya kubadilisha mtazamo wake juu ya kundi hilo kuwa ni kundi la kigaidi.

Msemaji wa ikulu ya Marekani Josh Earnest amesema kuwa mbali ya kutoona tofauti ya kundi hilo kwa kubadilisha jina lakini pia wanaamini kundi hilo linataka kushambulia nchi za magharibi.

Kundi la Al-Qaeda limethibitisha taarifa ya kundi hilo na kudai limekubali utengano huo.

Mmoja wa viongozi wa juu wa kundi la Al-Qaeda, Ahmed Hassan Abu al-Khayr, amesema kuwa kundi lake limetoa maelezo kwa uongozi wa Nusra Front kuendelea na kulinda haki za uislam na waislam nchini Syria.

Kwenye ujumbe huo pia kuna maneno machache ya kiongozi mkuu wa Al-Qaeda
Ayman al-Zawahri akisema: Undugu wa uislam ni imara zaidi kuliko uhusiano wa taasisi ambazo zinabadilika na kuondoka’

LEAVE A REPLY