Kumbe Irene Uwoya ndiyo chanzo Dogo Janja kuigiza kama mwanamke

0
207

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Dogo Janja amefunguka na kusema kuwa mke wake ndiye aliyemfanya uigize kama mwanamke kwenye video yake mpya ‘Wayu Wayu’.

Dogo Janja amesema mke wake ambaye ni muigizaji wa filamu za bongo, Irene Uwoya, ndiye alianza kumfanyia make up wakiwa mapumzikoni Zanzibar na kumvalisha vitu vya kike ndipo walipopata idea ya kufanya video akiwa kama mwanamke.

Amesema kuwa “Mke wangu kabla sijaanza kushoot alianza kunifanyia make up na kunivesha vesha tulipokuwa vacation (mapumzikoni) Zanzibar, akawa ananicheka, mpaka siku tunaenda kushoot ile make up ilibidi anifanyie yeye.

Kitendo cha Dogo Janja kuigiza kama mwanamke kimeonekana kuwakwaza watu wengi wakisema sio kitu kizuri mwanaume kuvaa hivyo na kujipodoa kama mwanamke, lakini kwa upande wake amesema ilikuwa ni ubunifu kwa lengo la kuboresha kazi.

LEAVE A REPLY