Kufuatia jaribio la mapinduzi, Uturuki yasitisha safari za nje kwa wasomi wa nchi hiyo

0
145

Nchi ya Uturuki imesimamisha kwa muda safari za nje kwa wasomi wa nchi hiyo, kama njia ya kuwakamata watu waliohusika katika jaribio la mapinduzi lililotokea wiki iliyopita.

Zaidi ya watu 50,000 wamekamatwa, kufutwa au kusimamishwa kazi wakiwemo walimu wapatao 21,000 ambao pia wanahusishwa kuhusika katika njama za mapinduzi ambapo zaidi ya 232 walifariki dunia.

Rais wa nchi hiyo, Recep Tayyip Erdogana amefanya kikao na maafisa usalama wa nchi hiyo na baraza lake la mawaziri na wakuu wa kijeshi wanaomuunga mkono tangu jaribio la kupindua serikali yake kufeli wiki iliyopita.

LEAVE A REPLY