Kubenea aitwa polisi kutoa maelezo baada ya kauli yake dhidi Profesa Lipumba

0
140

Mbunge wa jimbo Ubungo, Saed Kubenea ameitwa polisi leo kutoa maelezo kituo cha polisi kufuatia malalamiko aliyotoa mwenyekiti wa CUF, Profesa Lipumba.

Kubenea wiki iliyopita alifanya mkutano na vyombo vya habari kama Makamo Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani akiwa pamoja na baadhi ya viongozi wa CUF iliyochini ya uongozi wa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif na kutangaza oparesheni ya kumuondoa Profesa Lipumba katika ofisi za chama cha CUF Buguruni.

Baada ya Kubenea kutangaza oparesheni hiyo siku mbili mbele aliibuka Profesa Lipumba na kwenda kituo cha polisi kutoa malalamiko juu ya kile alichokisikia kutoka kwa kiongozi huyo na oparesheni hiyo aliyotangaza.

Profesa Lipumba na baadhi ya viongozi wa CUF wapo katika mgogoro kutokana na kiongozi huyo kipindi cha uchaguzi mwaka 2015 kuandika barua ya kujiuzulu nafasi yake kama Mwenyekiti wa CUF taifa na kubaki mwanachama wa kawaida badala yake amerudi tena.

LEAVE A REPLY