Koffi atua nchini apokelewa na Nandy

0
35

Mwanamuziki wa dance kutoka nchini Jamhuri ya Congo, Koffi Olomide amewasili Bongo usiku wa kuamkia leo, kwaajili ya kukamilisha collabo yake na African Princess Nandy.

Nandy amedokeza jina la ngoma hiyo kuwa ni ‘Leo leo’ na ameweka wazi kuwa yeye na timu yake wamefanya uwekezaji mkubwa sana kwenye project hiyo, hivyo mashabiki watarajie kitu kikubwa.

Koffi maarufu kama Mopao ametua nchini kwa lengo la kukamilisha kazi aliyoshirikiana na Mwimbaji wa hapa nchini ambapo wataingia studio na kufanya kazi yake hiyo.

Wawili hao walizungumza na vyombo vya habari hata kufichua jina la wimbo wao kuwa utaitwa Leo leo na hatua ya kushoot video ya wimbo huo nchini Tanzania.

Koffi na Nandy walionesha kuipa uzito mkubwa kazi yao hiyo iliyorekodiwa miezi kadhaa iliyopita hata kuwataka mashabiki kukaa mkao wa kula, kwani wamefanya kazi yenye viwango vya hali ya juu.

LEAVE A REPLY