Kocha wa Togo anusurika kifungo nchini Ufasansa

0
173

Kocha wa timu ya Taifa ya Togo, Claude LeRoy amenusurika kifungo badala amepigwa faini kwa kuhusika katika uhamisho wa uongo wakati alipokuwa kocha wa Racing Club de Strasbourg ya Ufaransa.

LeRoy, aliifundisha klabu hiyo, kati ya 1998 hadi 2003, ameagizwa na mahakama kuu ya Strasbourg kulipa pauni 12,790 (Takribani shilingi milioni 36.8).

Kocha huyo alidaiwa kujihusisha katika kughushi sahihi na majina ya uwongo katika uhamisho wa wachezaji wanne.

Kocha mkongwe kwasasa anaifundisha timu ya taifa ya Togo ambapo ameiwezesha kufuzu michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika yatakayofanyika nchini Gabon mwakani.

LEAVE A REPLY