Klabu bingwa Ulaya kuanza leo, Barcelona ‘uso kwa uso’ na Juventus

0
106

Michuano ya klabu bingwa barani Ulaya kwa msimu wa 2017/2018, utaanza leo rasmi kwa jumla ya michezo nane kupigwa katika viwanja mbalimbali.

Katika kundi A Manchester United watakuwa nyumbani katika dimba la Old Trafford kuwaalika Fc Basel, huku Benfica wakiwa wenyeji wa Cska Moscow.

Michezo ya kundi B Bayern Munich, wataanzia nyumbani nchini Ujerumani, kwa kucheza na wabeligiji wa Anderlecht, nao Celtic wakianza kwa kibarua kizito dhidi ya Paris Saint Germain.

Chelsea ya England wataanza kusaka ubingwa wa ulaya kwa kuwakaribisha Qarabag FK, waitaliano wa As Roma wataanza kwa kukipiga na Atletico Madrid, ikiwa ni michezo ya kundi C.

Miamba ya Catalunya Fc Barcelona watakuwa katika dimba lao la Nou Camp kukipiga na vibibi vizee Juventus , Olympiacos ya Ugiriki watapepetana na Wareno wa Sporting CP.

LEAVE A REPLY