Kivazi cha Zuchu chazua gumzo mtandaoni

0
75

Wasanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz na Zuchu wameibua maswali kibao kwa watumiaji wa mtandao wa Instagram baada ya wawili hao kuonekana wakiwa pamoja huku Zuchu akivalia kivazi kifupi ambacho kinaonyesha sehemu kubwa ya mwili wake.

Zuchu aliweka picha hiyo katika akaunti ya mtandao wake wa Instagram kitendo kilichozua mjadala kutoka kwa baadhi ya watumiaji wa mtandao huo.

Wafuasi wengi kwenye mtandao huo wameonyeshwa kuchukizwa na msanii huyo kuvalia kiguo kifupi mbele ya Diamond Platnumz ambaye ni boss wake kwenye muziki.

Wafuasi mpaka wamefika mbali na kusema kuwa uhenda wawili hao wakawa na uhusiano wa kimapenzi kutokana na ukaribu wao toka Zuchu alivyotambulishwa kama msanii wa WCB.

Kutokana na mashabiki hao kutoa comment mbaya kwenye picha hiyo mtandaoni Zuchu akaamua kuzima comment kwenye posti hiyo baada ya watu kumtolea manano machafu.

LEAVE A REPLY