Kitila Mkumbo ajiunga CCM rasmi

0
108

Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo amejiunga rasmi na Chama cha Mapinduzi CCM baada ya kujivua uanachama wa ACT-Wazalendo.

Katika taarifa iliyotolewa na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM, mkoa wa Singida, Martha Mlata imetuma salamu za kumkaribisha Katibu huyo.

Siku chache zilizopita Prof. Kitila Mkumbo alitangaza kujivua uanachama wa ACT Wazalendo akisema kuwa kitendo cha kuwa mwanachama wa ACT Wazalendo na kuwa Katibu Mkuu wa Wizara kuna mgongano wa kimaslahi, hivyo ni bora akashikilia upande mmoja.

Taarifa hiyo ilisema kuwa “Kwa niaba ya CCM mkoa wa Singida, namkaribisha Prof. Kitila Mkumbo kwa mikono miwili tuendelee kuimarisha chama cha mapinduzi katika mkoa wetu na taifa kwa ujumla, pia katika kusimamia na kuitekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa ustawi wa mkoa wetu na taifa letu,”.

LEAVE A REPLY