Kitendawili cha MH370 bado kigumu? New York Magazine laja na mapya

0
156
Ikiwa imepita takribani miaka miwili na nusu tangu kupotea kwa ndege ya Malasia, MH370, Sakinab Shah, dada wa aliyekuwa rubani mkuu Zaharie Ahmad Shah bado anaamini kuwa kaka yake ametumiwa kama kichaka cha kutupia lawama.
Ndege hiyo Malaysian Airlines Boeing 777, iliyopotea Machi 2014 iliua abiria wote 227 na wahudumu 12 waliokuwemo ndani yake.
Dada huyo amepinga ripoti mpya iliyotolewa na jarida la New York Magazine likidai kuwa kuna nadharia mpya inayoashiria kuwa rubani huyo alifanya kitendo cha makusudi kujiua ndani ya ndege hiyo akiwa na abiria.
Ingawa uchunguzi wa polisi wa Malysia haukugundua tatizo lolote la kifedha au tatizo binafsi, bado dada wa rubani huyo, Zaharie amejitokeza na kusema kuwa kaka yake ‘ametumiwa’ kama sehemu ya kutupia ‘visingizio’.
Ndege hiyo inadhaniwa kuzama kwenye kina kirefu cha bahari ya Hindi.
Kwenye mahojiano na shirika la habari la CNN, Zaharie amesema ‘Walifanya majaribio mengi mwaka 2014 ili kuutafuta ukweli lakini hakukuwa na ushahidi wa kumshuku kakaangu au harakati zake’
‘FBI walifanya majaribio yao na kama kungekuwa na chochote polisi wa Malaysia wangekuwa wa kwanza kufahamishwa. Ndio maana suala hili limeendelea kupuuzwa na vyombo vya usalama vya Malaysia’.
‘Ametumika kama kimbilio la visingizio tangu awali. Tuhuma hizi mpya, Mungu aepushe’
Viongozi wa Malaysia mara kwa mara wamekuwa wakikataa kutoa maoni yao juu ya kilichoandikwa kwenye jarida la New York Magazine.

LEAVE A REPLY