Kisa cha Diamond Platnumz kumualika Eric Omondi ‘All White Party’ hiki hapa

0
794

Unajua kuwa staa wa Bongo Fleva Diamond Platnumz anaweza kuwa ndiye staa aliyewafungulia milango mastaa wengi wa kimataifa nchini Tanzania?

Diamond ndiye aliyefungua milango kwa staa Jah Prayzah kupitia collabo yao ‘Watora Mari’ n.k

Miongoni mwa mastaa ambao wamefunguliwa mlango huo ni comedian wa Kenya, Erick Omondi ambaye pamoja na mambo mengine ameweka wazi namna Diamond Platnumz alivyolazimika kumfungulia milango.

Staa huyo alipewa kazi ya kuwa MC kwenye ‘All White Party’ ya Zari iliyofanyika Mlimani City na kudai chance hiyo haikuja hivi hivi.

Omondi amedai kuwa kilichomtoa nyoka pangoni mwa Diamond hadi kukubali kumpa kazi hiyo ni ngoma ‘Comedy version ya ngoma yake NASEMA NAWE ambayo yeye aliita NABEBA MAWE’.

Pamoja na ngoma hiyo, Omondi pia amefanya ngoma za JE UTANIPENDA ambayo ameiita JE, UTANIPEA? Na hivi karibuni aliachia SANG’OMBE ambaye ni refix ya SALOME.

Cheki video ya JE, UTANIPEA uone vituko vya Omondi.

LEAVE A REPLY