Kiongozi wa Korea Kaskazini apiga marufuku sherehe za krismasi

0
105

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un amepiga marufuku mikusanyiko inayoashiria kusherehekea sikukuu ya Krismasi kama vile inayohusu unywaji na uimbaji.

Ametaka wananchi kutosherehekea sikukuu hiyo na wanaopenda kufanya hivyo, waitumie Desemba 24 kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa bibi yake aliyezaliwa siku kama hiyo mwaka 1919.

Kiongozi huyo ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha vinadhibiti mikusanyiko yote ambayo inaendana na maadhimisho ya Krismasi.

Kim Jong Un amekuwa akichukua hatua kuzua kuenea kwa utamaduni kwa kigeni na amedhibiti vyombo vya habari kutotangaza taarifa zozote zinazoienzi sikukuu hiyo kama hatua ya kupiga marufuku Krismasi.

Ingawa sikukuu ya Krismasi si tukio kubwa nchini humo, lakini baadhi ya wananchi wamekuwa wakiisherekea na kufuata misingi ya Kikristo.

 

LEAVE A REPLY