Kinara wa unga nchini Tanzania, Ayub Mfaume atiwa mbaroni

0
444

Maafisa wa polisi nchini Tanzania wamesema kuwa wamemkamata kiongozi wa ulanguzi wa dawa ya kulevya aina ya heroine anayefanya shughuli zake kati ya Afrika mashariki na China.

Maafisa hao wanaokabiliana na ulanguzi wa dawa za kulevya wamesema kuwa Ayub Mfaume ambaye anajulikana kama kiboko alikuwa mmoja wa watu wanaotafutwa sana hapa nchini.

Anadaiwa kuwa na ushiirikiano na walanguzi wa dawa za kulevya nchini Brazil, Pakistan, na mataifa kadhaa ya Ulaya.

Maafisa hao wanasema kuwa Mfaume alijisalimisha kwa maafisa hao kufuatia msako wa wiki mbili dhidi ya walanguzi wa dawa za kulevya.

LEAVE A REPLY